Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mutamwega Mgaywa wa SAU amzungumzia Magufuli

Muta Mutamwega Mgaywa wa SAU amzungumzia Magufuli

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: ippmedia.com

Mgaywa amesema hayo wakati alipozungumza na Nipashe jijini Dodoma baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli.

Amesema tangu alipomfahamu Dk. Magufuli mwaka1995 walipoingia wote Bungeni anamkumbuka kwa maamuzi yake sahihi na yenye kusimamia maslahi sahihi ya nchi bila kubagua.

“Dk. Magufuli alikuwa ni Rais aliyejitoa kwa ajili ya wananchi na alitelekeza jambo sahihi kwa wakati lenye lengo la kuwanufaisha watu wake bila wonga wowote kwa vitendo” amesema.

Amesema kuanzia alipokuwa Naibu waziri wa ujenzi na baadaye kufanyakazi kwenye wizara tofauti akiwa waziri alifanyakazi kwa weledi na hakuwa mwoga katika kutekeleza jambo ambalo alikuwa akiamini kuwa linamaslahi ya nchi

Kadhalika, amesema kuwa hayati Dk. Magufulia alifanikiwa kuinua uchumi wa nchi kwa sababu aliwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu mhimu ambayo iliiwezesha kuingia kwenye uchumi wa kati .

Amebainisha kuwa yeye alimfahamiana na hayati Rais,Magufuli tangu mwaka 1995 wakiwa kwenye usafiri wa ndege kutoka Mwanza kuelekea Dar es salaam kuapishwa baada ya kuchaguliwa.

Chanzo: ippmedia.com