Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Must kuboresha elimu ya sayansi, teknolojia

Must kuboresha elimu ya sayansi, teknolojia

Mon, 16 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) Mkoa wa Mbeya kimesema kitaboresha utoaji elimu ya masomo ya sayansi na teknolojia katika nyanja ya ualimu ili kuwahamasisha watoto  kujikita katika somo la sayansi kuanzia elimu ya msingi, sekondari na vyuo nchini.

Mbeya. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must) Mkoa wa Mbeya kimesema kitaboresha utoaji elimu ya masomo ya sayansi na teknolojia katika nyanja ya ualimu ili kuwahamasisha watoto  kujikita katika somo la sayansi kuanzia elimu ya msingi, sekondari na vyuo nchini. Makamu Mkuu wa Chuo Must, Profesa Aloyce Mvuna amesema Jana kwenye mahafali ya saba ya chuo hicho ambapo wanafunzi 1,120 walihitimu katika ngazi ya shahada na stashahada. Amesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda masuala mengi yanahitaji teknokojia za kisasa na hivyo ni vyema kuwepo na mipango mikakati mizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. "Ni wakati sasa vyuo vikuu nchini kuona namna ya kuboresha nyanja ya ualimu kwa kuwepo kwa mitaala maalum ya masomo ya sayansi na teknolojia ili kudaili walimu wengi kwenye fani hiyo ambao watakuwa chachu ya kuhamasisha wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na kuiwezesha serikali kufikia azma ya uchumi wa viwanda," amesema. Profesa Mvuna pia amesema lengo la kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ni kuleta mabadiliko chanya ya mpango mkakati wa kuongeza soko la ajira nchini. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Zakia Meghji alisema katika kuboresha mitaala ya elimu serikali imepanua wigo wa kuboresha miundombinu hususan ujenzi wa maabara ya kisasa na hivyo kuwataka vijana waliohitimu wakawe chachu ya kutatua changamoto za wananchi vijijini na mijini kutokana na elimu waliyoipata. "Jamani elimu mliyoipata ikawe chachu katika kuibua changamoto za wananchi ikiwa ni pamoja na nyanja ya umeme, barabara na sekta nyeti ya kilimo ili kuunga mkono lengo la serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda," amesema Katika mahafali hayo mgeni rasmi alikuwa Spika wa Bunge mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Must, Pius Msekwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz