Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara, ambayo itahudumia wagonjwa wa rufaa kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, na nchi jirani kama Msumbiji, Zambia, Malawi, na visiwa vya Comoro.
Hospitali hiyo yenye sakafu tano, ujenzi wake umegharimu takribani bilioni 15 hadi kukamilika, na inakadiriwa kutoa huduma kwa wagonjwa 800-1,000 na kuwa na vitanda 1000 vya kulaza wagonjwa.
Huduma zitakazotolewa hospitalini hapo ni pamoja na upasuaji wa Jumla, tiba (Internal Medicine), matibabu ya moyo, matibabu ya watoto, tiba ya uzazi na via vya uzazi (Obstetrics and Gynaecology).