Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume asusia maziko ya mke, watoto wake wanne

85981 Pic+mume Mume asusia maziko ya mke, watoto wake wanne

Wed, 27 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Sengerema. Mvutano wa kifamilia umeibuka hadi kusababisha mume kususia maziko ya mkewe na watoto wake wanne.

Hali  hiyo imejitokeza jana Jumatatu Novemba 25, 2019 kwenye maziko ya watu watano wa familia moja waliopoteza maisha wilayani Sengerema mkoani Mwanza baada ya nyumba yao kuanguka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Novemba 23, 2019.

Maziko  ya watu hayo yalifanyika Kijiji Cha Kaswamwa wilayani Geita Mkoa wa Geita.

Mvutano huo umetokana na Zakaria Muhung'wa ambaye ni mjomba wa marehemu Veronica Magwenda kumnyima mume wa marehemu hao, Shinje Makenye kwenda kuwazika kwake Kijiji cha Kigumba wilayani Chato mkoani Geita.

"Ni kweli tulimnyima sababu alikuwa bado hajatoa mahari, pia walikuwa wametengana kwa miaka miwili sasa hivyo hakuwa na uhalali wa kuchukua miili hiyo kwenda kuzika kwake," alisema Muhung'wa

Akizungumza kwa Simu, Makenye amekiri kususia maziko kwa kuwa hawakustahili kuzikwa huko bali kijijini kwake.

Ni kweli nilikuwa sijatoa mahari lakini mahari siyo kigezo cha kunyimwa kuwachukua watoto wangu na mke wangu kwenda kuwazika, nimekwazika sana ila yote namuachia Mungu," alisema Makenye.

Alisema licha ya kutopata fursa ya kushiriki mazishi, lakini wameweka msiba kijijini kwao Kigumba wilayani Chato.

Chanzo: mwananchi.co.tz