Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muliro: Wananchi wa Dar hawataki wahalifu

Jumanne Muliro Dsm Muliro Jumanne Muliro

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa wananchi wa mkoa huo hawataki matukio ya kihalifu.

Muliro amesema hayo kufuatia maandamano ya baadhi ya wananchi ambao wanapinga mkataba wa uwekezaji wa bandari ya Dar kati ya Tanzania na Serikali ya Dubai.

"Wakazi wa Jiji la Dar es salaam ni watu ambao hawataki matukio ya kihalifu na hawakubaliani na vitendo vya kihalifu.

"Maandamano yakifanyika hayajifichi, huwezi kuwa mtu mmoja unatembea ukasema nimefanya maandamano, nadhani hata kwenye kamusi ukitafuta neno maandamano unaweza ukaelewa maana yake ni nini, usalama uliimarishwa kiwango ambacho kiliruhusu watu kufanya shughuli zao.

"Tulimjibu mhusika na tukampa pia ushauri kuwa kama ana hoja au jambo la msingi ambalo ni sehemu ya haki yake bado zipo mamlaka za kisheria ambazo angeweza kufikisha hoja zake bila kuathiri haki za msingi za kikatiba za watu wengine," amesema Kamanda Muliro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live