Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhimbili yatoa msaada wenye thamani ya Sh38 milioni Hanang

Manara Hananggggggg.png Muhimbili yatoa msaada wenye thamani ya Sh38 milioni Hanang

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupeleka msaada wa dawa, vifaa tiba pamoja Msaikolojia Tiba kwa wananchi wa Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang, Mkoani Manyara ili kusaidia jitihada za utoaji huduma.

Eneo hilo, lilikumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Hanang na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo vya watu 87, majeruhi, upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu.

Dkt. Yonazi amesema MNH imepeleka mchango ambao una aina mbalimbali (varieties) na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Akikabidhi dawa na vifaa tiba, Msaikolojia Tiba kutoka MNH Bi. Egla Fugusa amesema msaada huo una thamani ya TZS Milioni 38

Chanzo: www.tanzaniaweb.live