Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muheza wazindua anuani za makazi

BULEMBO MAKAZI Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Halima Bulembo

Sun, 6 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Halima Bulembo amezindua rasmi uwekaji wa anuani ya makazi huku akiwataka wananchi wilayani humo watoe ushirikiano kwa viongozi watakaopita katika maeneo yao kwaajili ya shughuli hiyo.

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Muheza mjini, Bulembo amesema kuwa anuani za makazi zitasaidia kutambua nyumba zote zilizopo wilayani humo.

Amesema kuwa uwekaji wa anuani za makazi utapita katika kata zote 37 za wilaya hiyo ambapo nyumba zote zitawekewa namba.

Mratibu wa Kamati ya Anwani ya Makazi wilayani humo, Mkunbo Ngoi amesema kuwa tayari watendaji wa kata 37 na vijiji 126 wameshajengewa uwezo.

"Uhamasishaji wa uwekaji anuani za makazi kwa ngazi ya vijiji na vitongoji umefanyika kupitia watendaji na tayari wameainisha barabara zilizopo na utoaji majina kwa barabara zisizo na majina" amesema Mratibu huyo.

Baadhi ya wananchi wa Wilaya hiyo wameipongeza Serikali Kwa kuuamua kuanza kuweka anuani za makazi na kwamba litasaidia kuondoa usumbufu hasa kwa wafanyabishara na wageni.

Advertisement Mkazi wa Muheza mjini, Hassan Mngumi amesema mchakato huo umekuja muda muafaka na anuani hizo za makazi anuani zitarahisha mambo mengi.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz