Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muheza kupanda miti milioni 1.5

Hali Bulembo akipanda mti

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imeadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kupanda miti 600 katika kata ya Lusanga ikiwa ni mkakakati wa kufikia lengo la kupanda miti milioni 1.5 wilayani humo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo leo Jumanne Aprili 26, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Muheza (DC), Halima Bulembo amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo muhimu kwa kupanda miti lengo ni kutaka kuenzi Muungano huo kwa kudumisha amani na upendo kwa wananchi.

Bulembo amesema katika maadhimisho haya wamepanga kupanda miti million 1.5 katika kata 37 za Wilaya ya Muheza ambapo watapanda miti ya matunda, kivuli na urembo.

Mkuu wa Wilaya huyo alitumia fursa hiyo kuwashukuru Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Msitu wa Lunguza na Tari Mlingano kwa kuwapatia miche hiyo ya miti.

Baadhi ya wakazi wa Kata ya Lusanga wamesema kuwa watailinda na kuitunza miti hiyo ambayo imepamdwa leo katika sherehe za maadhimisho ya Muungano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live