Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mufindi yavuka lengo ukusanyaji wa mapato

Mufindi Mapato.jpeg Mufindi yavuka lengo ukusanyaji wa mapato

Sun, 28 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato yake ya ndani kwa zaidi ya asilimia 100 ambayo walikuwa wamejipangia kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni 30 mwaka huu.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Festo Mgina amesema wamefanikiwa kuvuka lengo na kukusanya asilimia 126 kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya watalaamu na madiwani hao.

"Tumefanikiwa kufikia asilimia 126 kwa sababu ya ushirikiano mzuri uliopo baina yetu hivyo nichukue fursa hii kuwapongeza madiwani wenzangu na wataalamu kwa juhudi kubwa ambayo wameionyesha ya ukusanyaji wa mapato hadi kufikia asilimia hizo." amesema Mgina

Mwenyekiti huyo amesema kuwa wafanyabiashara wamekuwa wanalipa ushuru ambayo ndio mapato ya halmashauri kwa moyo mmoja hali ambayo imesaidia kuweza kuvuka kwa lengo ambalo walikuwa wamejipangia.

Pia, Mwenyekiti huyo amezungumzia namna ambavyo wataweza kukusanya mapato kwa mwaka ambao umeanza licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

"Changamoto iliyopo kwa mwaka huu wa fedha ambao umeanza namna ambavyo wafanyabiashara hawajitumi kulipa kodi kwa hiari kwa sababu mfumo wa ukusanyaji wa ushuru wa mapato ya ndani umekuwa na mabadiliko kutokana na sheria ambayo imebadilishwa na Bunge na kuletwa utaratibu mwingine wa ukusanyaji wa mapato hayo kutoka asilimia 0.5 hadi 0.3." amesema Mwenyekiti huyo.

Amesema mabadiliko hayo yamekuja wakati tayari makisio ya bajeti ijayo imeshapitishwa hivyo imekuwa changamoto kwa halmashauri hiyo huku akieleza namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha wanakusanya mapato hayo kama walivyokusudia.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itandula, Iddi Mabena amesema kuwa uchumi wa Halmashauri hiyo inategemea mazao ya misitu.

"Malengo haya yalikuwa kukusanya zaidi ya asilimia 126 ama zaidi ya hapo lakini hata hapo tulipofikia bado sio mbaya ila tunaimani tunaweza kwenda mbele zaidi ya hapo ili kuhakikisha halmashauri unapata mapato Makubwa na kufanya vitu vyao vya msingi ambavyo wamejipangia."amesema Mabena

Chanzo: Mwananchi