Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtwara watumia TSh bilioni 1 elimu na utawala bora

92c0a397a65ed255214767fb039875bb.jpeg Mtwara watumia TSh bilioni 1 elimu na utawala bora

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya elimu na utawala bora iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni moja.

Miradi hiyo ni lipa kwa matokea (EP4R) pamoja na miradi ya usafi na mazingira shuleni (SWASH).

Ofisa Habari na Mawasiliano, Isack Bilali alisema mradi wa SWASH uliotekelezwa mwaka wa fedha 2019/20 ulijenga matundu ya vyoo 128 katika shule saba za msingi ambazo ni Msangamkuu, Mnete, Miuta, Libobe, Mkonye, Kitere na Nakada yaliyogharimu milioni 178.

Bilali alisema katika mwaka wa fedha 2020/21 walijenga madarasa 21 katika shule nane ikiwemo Mpapura, Libobe, Naumbu, Tangazo, Msangamkuu, Ilala, Msijute na Dihimba Fedha zilizotokana na mradi wa lipa kwa matokeo (EP4R) kwa Sh milioni 414.1.

Aidha Bilali alibainisha mwaka wa fedha 2020/21 walitekeleza mradi wa ujenzi wa matundu ya vyoo 204 katika shule 11 za msingi ikiwemo Mkunwa, Likonde, Namanjele, Ming’wena, Mkubiru, Tangazo, Nachenjele, Madimba, Mayaya, Mbuo na Chemchem iliyogharimu Sh milioni 272.8 pamoja Sh milioni 693 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala ambalo ujenzi unaendelea.

Aidha Bilali alisema halmashauri hiyo kwa mwaka 2021/22 wanatarajia kupokea milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi 15. Makamu Mkuu wa shule ya sekondari ya Sabodo, Mwalimu Kurwa Husein alisema shule ni hapo walipokea miradi miwili ya lipa kwa matokeo (EP4R) ambapo walipokea Sh milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana na Sh milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Msijute, Salumu Natenda alisema kutekelezwa kwa mradi wa lipa kwa matokeo (EP4R) shuleni kumepunguza uhaba wa vyumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live