Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtumishi kufukuzwa kwa ulevi

94141 Mtumishi+pic Mtumishi kufukuzwa kwa ulevi

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbarali. Baraza la madiwani wilayani Mbarali mkoani Mbeya limeazimia kumfukuza kazi mtumishi mmoja kwa kwa tuhuma za ulevi wa kupindukia.

Imeelezwa kuwa mtumishi huyo awali alikuwa idara ya afya na alishusha cheo kutokana na tatizo la ulevi.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi alisema mtumishi huyo ni miongoni mwa wengine watatu watatu ambao wameonywa mara kwa mara kuhusiana na ulevi kazini.

“Kimsingi uamuzi wa madiwani si kuonea bali ni jukumu lao kwa kuwajibisha watumishi kwani alionywa mara kadhaa lakini imeshindikana mpaka tukafikia hatua ya kumshauri tumpe uhamisho akafanye kazi mkoani kwao Kigoma, lakini hakuonyesha ushirikiano,” alisema.

Naye mkuu wa wilaya hiyo, Reuben Mfune alisema ni jambo la kusikisha kwa mtumishi wa Serikali kuacha kazi kwa ulevi.

“Uamuzi wa baraza siyo wa kulaumiwa kwani huyo mtumishi alionywa lakini alishindwa kubadilika, nawapongeza madiwani kwa kuhamashisha uchangiaji maendeleo kwa wananchi,” alisema.

Pia Soma

Advertisement
akizungumzia uamuzi huo, ofisa utumishi wilaya, Aswege Kaminyoge alisema umefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina sambamba na mhusika kuhojiwa na kuonywa mara kwa mara.

Baadhi ya watumishi walisema uamuzi huo ni mgumu lakini hakuna namna.

Chanzo: mwananchi.co.tz