Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa wa wizi wa bodaboda akutwa amechinjwa

Mauaji?fit=600%2C400&ssl=1 Mtuhumiwa wa wizi wa bodaboda akutwa amechinjwa

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoani Songwe linawasaka watu waliofanya mauaji ya watu wawili akiwemo kijana Feston Mgalla (27) mkazi wa kijiji cha Igamba wilayani mbozi aliyechinjwa na mwili wake kutupwa barabarani.

Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Songwe, Rashidi Ngonyani amesema kuwa mwili wa kijana huyo uliokotwa majira ya saa 12:00 asubuhi ukiwa umechinjwa na kutupwa barabarani.

“Alikutwa ameuawa kwa kuchinjwa na baadaye kutupwa barabarani, taarifa za awali zinaonyesha kijana huyu alikuwa akijihusisha na wizi wa bodaboda. Hakuna watu waliokamatwa na tunaednelea kufutailia,” amesema kamanda Ngonyani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live