Siku moja baada ya kuripotiwa juu ya Mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki, Abdul Bonge aliyekuwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani, Tabata, Kinyerezi jijiniDaresSalaam, kuchukuliwa kwa nguvu na waendesha Bodaboda, Mwili wake umepatikana maeneo ya #Vingunguti na unatarajiwa kuzikwa leo Agosti 5, 2023.
Mwanafamilia wa Marehemu amesema, "Mwili ulipatikana juzi (Agosti 3) taratibu za Kipolisi zikafanyika na wakatukabidhi, Mama Bonge alipopata taarifa wakati purukushani zinaendelea akajua siku ya Mwanaye imefika, ni kama alishajiandaa Kisaikolojia kutokana na Matukio ya nyuma.”
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa #Kichangani, Leonard Nyukuli amesema, baada ya Bodaboda kuvamia Ofisi yao na kuwazidi nguvu waliita Polisi na kwa bahati mbaya hawakufika kwa muda muafaka.
Tukio la wizi lilivyokuwa Inaelezwa kuwa, usiku wa kuamkia Agosti 3, dada mmoja ambaye hajatambulika alimchukua Bodaboda kutoka Kinyerezi Sokoni (Mnadani) majira tano usiku, ampeleke Kichangani Darajani.
Baada ya kushuka abiria akatoa Tsh. 10,000, wakati dereva wa Bodaboda anatafuta chenji, ndipo wakatokea watu wawili na kumshambulia, katika purukushani dereva akitaka kuchmoa funguo wakampiga na kitu kizito usoni na kisha kumtupa kwenye mtaro.
Baada ya muda dereva Bodaboda akaenda kuomba msaada nyumba ya jirani ambapo wakatoa taarifa kwa Mjumbe wa Mtaa kisha kupelekwa katika moja ya zahanati ya Kinyerezi.
Usiku huohuo taarifa zikaanza kusambaa juu ya kilichotokea, ndipo mtu mmoja akasema amemuona Bonge akiwa anakokota pikipiki.
Wavamia nyumbani kwa Bonge Inadaiwa Bonge ni mwizi maarufu maeneo hayo na kutokana na rekodi yake ya nyuma vijana wengi wa Bodaboda walikuwa na kisasi naye na walikuwa wakisubiri ‘ajichanye’.
Wakiongozana na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichanganyi,….. wakafika nyumbani kwa Bonge ambaye baada ya kubanwa akakiri kuiba pikipiki husika, akaenda kuonesha alipoificha, kisha akachukuliwa kwenda kuhifadhiwa katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa, akiwa pamoja na kijana ambaye alijeruhiwa na kuporwa pikipiki.
Bodaboda wavamia Ilipofika alfajiri, kundi la Bodaboda zaidi ya 30 wakavamia ofisi hiyo wakimtaka mtuhumiwa kwa kuwa ni kawaida yake kufanya matukio na kuachiwa.
Nguvu iliyotumika ikawazidi nguvu viongozi wa Serikali za Mtaa, wakafanikiwa kumtoa Bonge na kutokemea naye kusikojulikana huku mashuhuda wakidai walielekea njia ya Gongo la Mboto.
MWENYEKITI WA MTAA Mwenyekiti Serikali ya Mtaa ya Kichangani, Leonard Nyukuli alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema "Nipo nje ya ofisi, kama unataka taarifa zaidi njoo ofisini utapata taarifa rasmi ya kiofisi."
MWILI WA BONGE WAPATIKANA Mwanafamilia wa marehemu (jina linahifadhiwa) amesema mwili ulipatikana maeneo ya Vingunguti, juzi (Agosti 3), Mama Bonge tumezungumza naye amesema alipopata taarifa za tukio akajua siku ya mwanaye imefika hata kabla ya kuupata mwili, ni kama alishajiandaa kisaikolojia kutokana na matukio ya nyuma.”
Naye, Mwenyekiti wa Kichangani, Leonard Nyukuli amesema "Wananchi waache kujichukulia Sheria mkononi, mtuhumiwa alitoa ushirikiano akaonesha pikipiki, kuna watu waliotoka sehemu nyingine ndio wakafanya hayo waliyofanya, tuliita Polisi hawakufika kwa muda muafaka ndio yakajitokeza hayo."