Mkazi wa Bunda mkoani Mara, Webilo Nyakolo (32) amefariki dunia baada ya kuangikiwa na gema wakati akiwa katika machimbo ya dhahabu ya Halawa wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Ajali hiyo imetokea jana Julai 4 2022 alfajiri ikuhusisha duara mbili zilizopo katika mgodi wa John Stephan Luhende & Partners ambayo ilikuwa chini ya uangalizi wa mafundi.
Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Madini Mkoa wa Simiyu, Amin Msuya amewaambia wandishi wa habari kuwa wasaidizi wa mafundi walikuwa wanatoa magema ambayo yanakuwa yameshika kwenye miamba ya maduara ili waweze kufunga mitambo.
"Kwenye kutoa magema, gema moja wapo liliwaangukia mafundi na kusababisha ajali, kwa sasa shughuli za uchimbaji zinaendelea na majeruhi wawili wanelazwa katika hospitali ya Songambele Nkololo," amesema Msuya.
Majeruhi katika ajali hiyo ni Baraka Kigoyi (32) mkazi wa Kijiji cha Hunyari wilaya ya bunda Mkoa Mara na Shata Masuke (40) mkazi wa Kijiji Cha Girya kata wilaya ya Bariadi mkoani SimiyuÂ