Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa miaka 12 abakwa akitoka kwenye harusi

Ewf Mtoto Mtoto wa miaka 12 abakwa akitoka kwenye harusi

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa miaka 12 mkazi wa Kijiji cha Dilifu Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi (jina limehifadhiwa) amesimulia jinsi alivyolawitiwa huku mlezi wake akiomba msaada wa serikali ili mtuhumiwa huyo achukuliwe hatua stahiki.

Ilikuwa majira ya jioni wakati mtoto huyo alipokuwa akitoka kwenye sherehe ya harusi ndipo alipokumbana na mwanaume mmoja aliyemfanyia unyama huo.

“Nilikuwa natoka kule, nikafika hapo akanikamata mkono, akanipiga mtama kisha akaanza kuniburuza. Aliponifikisha mbele kule akaniambia piga magoti, nikakataa ndipo akanikaba kooni nikashindwa kupiga kelele kuomba msaada, akanilaza chini na kunifanya tukio,” amesema mtoto huyo.

Aidha kwa upande wa mama mlezi wa mtoto huyo amesema hapo mwanzo hakuelewa afanye nini baada ya kuletewa mtoto wake na uongozi wa kijiji akiwa kwenye hali mbaya.

“Nikaona mtoto wanamleta, mimi nilijua yupo pale kwenye sherehe, nikamuuliza ulikuwa wapi, akajibu tu hovyo hvoyo alikuwa amechokachoka, baadaye akasema mimi nimebakwa,” amesema mama huyo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Dilifu amesimulia tukio hilo na namna ambavyo mtuhumiwa huyo alivyokamatwa baada ya kutoroka alipomaliza kutekeleza unyama huo.

“Mtuhumiwa alipofikia ni kwa balozi wa nyumba kumi, balozi naye alikuwa kwenye maandalizi ya kuja kwenye windo la kumtafuta huyo mtu, balozi akamkaribisha akaomba chakula, akapewa akala. Akaomba asaidiwe pa kulala, wakamwambia hakuna shida.

“Balozi akakusanya majirani zake kulea, wakasogea, walipofika pale wakasema mtu wetu ambaye tulikuwa tunaenda kwenye lindo ndiyo huyu ambaye amejileta mwenyewe,” amesema Mwenyekiti.

Aidha, juhudi za kulitafuta Jeshi la Polisi mkoani Katavi zinaendelea ili waweze kuzungumzia taarifa za tukio hilo na uchunguzi ulipofikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live