Yusra Hassan Ally, mwanafunzi wa darasa la pili kutoka kata ya Nyengedi, Halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi, amejinyonga hadi kufa kwa kutumia nguo ambapo mpaka sasa sababu za uamuzi huo hazijafahamika
Taarifa ya jeshi la polisi Mkoani Lindi iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Afisa Mnadhimu wa jeshi hilo Kamishna msaidizi wa Polisi, Alhaji Kabaleke, imesema tukio hilo limetokea Mei 17 majira ya saa nane mchana katika kata ya nyengedi Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.
Alhaji kabaleke amesema kuwa, binti huyo mwenye umri wa miaka 11 alikuwa akiishi na bibi yake, ambapo siku hiyo alishindwa kwenda shule kwa kisingizio kuwa anaumwa, ambapo aliweza kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kufua nguo zake
Alisema baada ya kumaliza kazi hizo binti huyo alionekana akichukua nguo na ndoo na kuamua kujitundika kwenye mti hadi kifo chake.