Mara. Kasobi Shida (26) ambaye ni mtoto wa dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara amefariki dunia.
Kasobi alilazwa hospitalini hapo Jumapili Agosti 4, 2019 baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari linalotumiwa na baba yake, Shida Masaba (55) kumwendesha Mkuu wa Mkoa.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk Hosea Bisanda akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Agosti 6,2019 amethibitisha kutokea kwa kifo hicho usiku wa kuamkia leo.
Dk Bisanda amesema taarifa kamili bado hajapata kwa vile hajafika hospitalini.
Soma zaidi: Dereva wa gari ya RC iliyopata ajali analia kila mara
Pia Soma
- Usajili wa Simba, Yanga gumzo
- Simba, Yanga zawarudisha uwanjani Mziba, Kibadeni
- Ubora wa kikosi Simba uko hapa
- Bigirimana, bunduki mpya Yanga inayomuota Ajibu
Soma Zaidi: Gari la RC Mara lapata ajali likidaiwa kuendeshwa na mtoto wa dereva wake
Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu ya Mwananchi