Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwingine ashambuliwa na fisi Bariadi, ajeruhiwa vibaya

Mtoto Fisi.jpeg Mtoto mwingine ashambuliwa na fisi Bariadi, ajeruhiwa vibaya

Mon, 2 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matukio ya Fisi kushambulia watoto na kuwajeruhi vibaya maeneo ya usoni na kichwani yamezidi kushamili katika mji wa Bariadi, ambapo mapema asubuhi ya leo mtoto mwingine jina ni Gindu Kululu (06) mkazi wa mtaa wa Iyoma kata ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi ameshambuliwa na myama huyo.

Wazazi wa mtoto huyo wanaeleza kuwa majira ya Saa 8:00 kamili Asubuhi nyumbani mtoto huyo akiwa na mdogo wake nje, gafla alivamiwa na fisi huyo ambaye alitokea vichaka vilivyopo karibu na nyumbani.

Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji wa Bariadi Emmanuel Costantine amethibitisha kupokelewa kwa mtoto huyo na hali yake ilivyo.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange akiwa na kikosi cha Askari wa kutuliza gasia (FFU) walianza msako wa kumtafuta fisi huyo na kumpata hadi kumuua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live