Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwenye ualibino aibiwa Muleba

Ualibinoo 02 Mtoto mwenye ualibino aibiwa Muleba

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kagera juzi, Jumamosi Juni Mosi, limewahoji wazazi wa mtoto Asimwe Novarti mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) aliyeibwa katika Kitongoji cha Mbale, Kijiji cha Bulamula wilayani Muleba na watu wasiojulikana mpaka sasa na kisha kutokomea na mtoto huyo.

Mara baada ya mahojiano hayo na polisi, mama mzazi Judith Kebyera Richard aliachiwa huru huku Baba mzazi Novath Venant akiendelea kushikiliwa katika Kituo cha Wilaya ya Muleba.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili na nusu aliibwa nyumbani kwao Mei 30 mwaka huu, baada ya watu wasiofahamika kubisha hodi na kumlaghai mama wa mtoto huyo Judith Kebyera Richard kuwa wanaomba msaada, wakidai mmoja wao aligongwa na nyoka.

Akisimulia mkasa huo mama wa mtoto amesema ilikuwa ni saa 2:30 usiku siku ya Alhamisi baada ya kuitwa na watu hao wakiomba msaada kwa kumtaja jina na ndipo alipoamua kutoka na mfuko wa chumvi na kuanza kummiminia mmoja wao na wakati akitoa msaada huo kijana mmoja wa wahalifu hao alimkaba na mwingine aliingia ndani na kumkwapua mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live