Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto mwenye Ualbino anusurika kifo Geita

Albinoo Mtoto mwenye Ualbino anusurika kifo Geita

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye ualbino, Kazungu Julius (9) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Katoro wilayani Geita amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa sehemu za kichwani, mkononi na kidole cha mkono aliposhambuliwa na mtu asiyejulikana kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo amesema tukio hilo lilitokea Mei 4 mwaka huu saa mbili usiku katika Mtaa wa Mtakuja Mamlaka ya Mji mdogo Katoro.

Amesema mtu mmoja ambaye hajajulikana alimvizia mtoto huyo akitoka chooni na kuanza kumshambulia na kitu chenye ncha kali, hali iliyosababisha majeraha makubwa mwilini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live