Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto atumbukia kwenye sufuria yenye chai, afa

33f1aee64512177d0c3041531b8733c2 Mtoto atumbukia kwenye sufuria yenye chai, afa

Fri, 24 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MTOTO Nanzia Samwel (6), wa darasa la kwanza katika shule ya St Anne Marie iliyopo Mbezi kwa Msuguli, jijini Dar es Salaam ametumbikia kwenye sufuria yenye chai ya moto na kufa.

Mtoto huyo baada ya kuungua, alikimbizwa hospitalini na alipozinduka, kwa sauti iliyotoka kwa shida, alisema: “Yesu nisaidie maumivu makali niliyonayo,” kisha muda mfupi baadaye, akakata roho.

Mama mkubwa wa mtoto huyo, Happiness Mtenga alilieleza gazeti hili jana kuwa, baada ya Nanzia kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na mama yake akitokea Hospitali ya Bochi, alikuwa amezimia na alipozinduka alimweleza mama yake, Lucia Mtenga kuwa ana maumivu makali na mama yake alimwelekeza amwite Yesu amsaidie.

Chanzo: habarileo.co.tz