Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto atelekezwa Ngara

32103 Pic+mtoto TanzaniaWeb

Tue, 18 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ngara. Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne ameokotwa leo Jumatatu Desemba 17, 2018 baada ya kutelekezwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Fele.

Mtoto huyo ametelekezwa katika uzio wa kituo cha Redio Kwizera wilayani Ngara mkoani Kagera.

Akizungumza na Mwananchi leo Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ngara, Abeid Maige amethibitisha kupokea taarifa za kuokotwa kwa mtoto huyo.

Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa majina ya Esta Masabo amesema alikuwa na kijana wa kiume anayesoma Shule ya Msingi Nyamiaga, wilayani Ngara.

Mmoja wa wafanyakazi wa redio hiyo, Godwin Buchard ndiye aliyewafahamisha wenzake kuwa mtoto huyo alikuwa na kijana mmoja aliyekuwa akizungumza na simu kisha kutokomea kusikojulikana.

Kaimu ofisa ustawi wa jamii wilayani humo, Debora Kasomwa amesema amempeleka mtoto huyo kituo cha polisi Ngara mjini kuandikisha maelezo ili wakijitokeza wazazi wake aweze kutambulika.

"Wazazi hawana budi kuwalea watoto kwa kuwafundisha kutaja majina yao na wanaoishi nao ili kuweza kutambulika kwa urahisi,” amesema Kasomwa.

Mtoto huyo amewataja watoto wenzake anaocheza nao nyumbani kwao kuwa ni Dorisi, Eva, Paschal na Ailine,

Namba ya kumpata Kasomwa ni 0787070938.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz