Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto aliyesaidiwa na Waziri Mkuu afariki akipatiwa matibabu

Kifoo Mtoto Mtoto aliyesaidiwa na Waziri Mkuu afariki akipatiwa matibabu

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto Zahir Akili aliyesaidiwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kupata matibabu ya ugonjwa wa moyo baada ya mama yake kuandika karatasi ya kuomba msaada wa gharama za matibabu kwa Majaliwa alipokuwa ziarani mkoani Mtwara, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Matibabu ya mtoto huyo aliyefariki akiwa anafanyiwa vipimo yalikuwa yanagharimu zaidi ya Sh28 milioni.

Akizungumza nasi wakati wa mazishi ya mtoto huyo jana Jumamosi Julai 15, 2023 Mohamed Luyenda (babu wa mjukuu upande wa mama) amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kumsikiliza binti yake na kumsaidia matibabu ya mtoto wake.

“Unajua Yule Zahir ni mjukuu wangu alizaliwa akiwa na matatizo tulihangaika nae sana alipata matibabu nusunusu kutokana na uwezo mdogo, hali ambayo ilitupa wakati mgumu sana. Lakini ujio wa Waziri Mkuu kwetu ulitupa faraja na msaada alioutoa kwetu ulitupa matumaini mapya lakini Mungu anapanga lake leo, tumemzika mjukuu wangu,”amesema kwa huzuni.

Huku Abdu Akili (babu wa Zahir upande wa baba) amesema kuwa walipata taarifa kuwa Zahir amefariki akiwa anafanyiwa vipimo.

“Jana jioni hali ya mtoto ilibadilika na alifariki akiwa bado hajapatiwa matibabu stahiki kwakuwa ndio kwanza alikuwa anaingia kwenye vipimo tunashukuru kwakuwa lengo la Waziri Mkuu lilikuwa zuri, kama si yeye sisi tungeumbuka kwakuwa mtoto huyo alikuwa na hali mbaya sana,” amesema Mzee Akili

Aisha Luyenda mama wa mtoto huyo alitoa ombi la mtoto kupatiwa matibabu kwa njia ya maandishi katika ziara ya waziri mkuu mkoani hapa, wakati kiongozi huyo akipita katika Kijiji cha Nanguruwe ambapo alisema kuwa mtoto huyo alibainika kuwa na tatizo la moyo kuelekea upande wa kulia wa kifua badala ya kushoto (Dextrocardia) na kwamba anahitaji matibabu makubwa zaidi lakini hana uwezo wa kuyagharamikia.

Ambapo Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ambaye pia alikuwa katika ziara hiyo alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hamad Nyembea kumuandaa mtoto huyo kwa ajili ya kumpa rufaa kwenda kutibia Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa gharama za Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live