Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto aliyeondolewa damu kwenye ubongo, arejea masomoni

Mtoto Ubongo Mtoto aliyeondolewa damu kwenye ubongo, arejea masomoni

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mtoto Sheimaa Shaibu (9) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kwale Manispaa ya Mtwara Mikindani, aliyepata ajali ya kugongwa na pikipiki Mei mwaka huu na kufanyiwa upasuaji na madaktari wa Hospitali ya Kanda ya Kusini amerejea masomoni.

Akizungumza na Mwananchi shuleni hapo, Sheimaa amesema kuwa siku ya tukio alikuwa anatokea madrasa ambapo aliona bajaji ikiwa imesimama kama ishara ya kumpisha, alipopita alishtukia anagongwa na pikipiki.

“Kwa kawaida tnapotoka madrasa, huwa tunasindikizwa hadi barabarani na tunavukishwa, lakini siku hiyo mimi nilikuwa mbali naongea na wenzangu, hivyo sikuwepo kati ya wale waliovushwa barabara, jambo lililosababisha mimi kupata ajali nikiwa najaribu kuvuka barabara,” amesema Sheimaa Also Read

Wawili wafariki ajali ya basi Kibaha Kitaifa 7 min ago Wawili wafariki ajali ya basi Kibaha Kitaifa 7 min ago

Nae Khadija Abdallah (Mama wa Sheimaa) amesema kuwa mtoto huyo amepona na amerejea katika hali yake ya kawaia na kwamba anaendelea na masomo yake kama ilivyokuwa awali.

“Baada ya ajali mtoto alikuwa anajinyonganyonga…tukaambiwa kuwa damu imechanganyikana na ubongo kwa kasi kubwa, hali ambayo ilipelekea apumzishwe, lakini baadae tulipewa rufaa kwenda Hosptali ya Kanda ya Kusini ambapo alifanyiwa upasuaji,” amesema Khadija na kuongezwa;

“Kwetu tunaona kama ni muujiza, madaktari wetu walikuwa na umakini, yaani haikuchukua mwezi vidonda vilipona na akawa vizuri, tunashukuru Mwenyezi Mungu.”

Kwa upande wake Dk Hashimu Tito, aliyeongoza jopo la upasiaji kutoka katika hospitali hiyo, amesema kuwa upasuaji huo ulikuwa wa kwanza na wenye mafanikio makubwa kwa mtoto wa miaka 9 aliyepata ajali.

“Zoezi la kutoa damu iliyovilia kwenye ubongo wa mtoto mdogo baada ya kupata ajali, lilifanyika kwa utaalam mkubwa na kwakweli lilifanikiwa, awali tulifanya vipimo na uchunguzi na ikagundulika kuwa na damu kwenye ubongo iliyovilia baada ya kupata ajali ya kugongwa na pikipiki,” alisema Dk Tito.

Chanzo: mwanachidigital