Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto ajiua kisa nguo za sikukuu

Mauaji DRC Crime Scene Mtoto ajiua kisa nguo za sikukuu

Thu, 29 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13, Zamada Jafari, Mwanafunzi wa darasa la nne katika Kijiji cha Ikengwa Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mtandio wa Mama yake chanzo kikiwa ni kukosa nguo za Sikukuu.

Tukio limetokea June 27, 2023 saa 10 jioni ambapo Babu yake alijaribu kumuokoa lakini usafiri wa kumpeleka Hospitali ulikosekana hivyo alifia nyumbani na mwili wake umezikwa jana June 28, 2023.

Baada ya kufika kijijini hapo kuongea na Wazazi wa Marehemu pamoja na Uongozi wa kijiji hicho ambapo Baba wa Marehemu amesema;

“Siku ya tukio nilikuwa mnadani ndipo nikapata taarifa hizi lakini Wadogo zake wanasema Dada alisema atajinyonga maana hajanunuliwa nguo za Sikukuu, ni kweli tulikubalina kwamba nitamnunulia nguo za Sikukuu lakini pesa haikutosha"

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ijumaa Mohamed amewaomba Wazazi pindi Mtoto anapokuwa na uhitaji na Mzazi ana uwezo basi asisite kumsikiliza ili kuwapa Watoto furaha huku akisema Watoto hawapaswi kuchukua maamuzi ya namna hiyo kwa kuwa hali ya uchumi kwa sasa ni ngumu na nguvu kubwa inaelekezwa katika chakula.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live