Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto afariki ndani ya shimo

68971 Pic+mtoto

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mtoto mwenye miaka saba, Steven Marwa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Nyansurura wilaya ya Serengeti amefariki dunia baada ya kuzama ndani ya shimo la maji.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Nurdin Babu leo Jumanne Julai 30, 2019  amesema tukio hilo limetokea jana Jumatatu majira ya saa 10 jioni na mwili uliopolewa na wananchi baada ya mama yake mzazi aliyekuwa anafua eneo hilo kupiga yowe.

Ofisa elimu kata hiyo, Odongo Kagose amesema mama yake ambaye ni mjamzito alipoteza fahamu baada ya kushuhudia mtoto wake akizama bila msaada.

"Wakati mama yake anafua mtoto alikuwa akicheza pembeni mwa shimo hilo ambalo lilichimbwa na kampuni Gemen Engineering kwa ajili ya molamu, ghafla akaanguka kwa kutanguliza kichwa kwenye tope akashindwa kujinasua," amesema.

Amesema mazishi yanatarajiwa kufanywa nyumbani kwa leo Jumanne Julai 30, 2019 baada ya taarifa za polisi kukamilika.

Chanzo: mwananchi.co.tz