Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mto wafurika maji, msafara wa RC Songwe wakwama

40794 Mkurugenzipic Mto wafurika maji, msafara wa RC Songwe wakwama

Mon, 11 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songwe. Msafara wa mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali mstaafu, Nicodemus Mwangela umelazimika kusimama kwa muda kusubiri maji ya mto Ngumba kupungua ili uweze kuendelea na safari.

Mkuu huyo wa Mkoa alikuwa akitokea makao makuu ya Mkoa Vwawa wilayani Mbozi kuelekea eneo la Mkwajuni halmashauri ya Wilaya ya Songwe kwa ajili ya uzinduzi wa mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa.

Msafara huo umekwama leo Ijumaa Februari 8, 2019 kuanzia saa 12 asubuhi na hadi kufikia saa 5 asubuhi bado magari yalikuwa eneo hilo.

Wakazi wa eneo hilo wamesema mto huo hujaa maji kila inaponyesha mvua kubwa na kufanya mawasiliano kati ya pande mbili zinazotenganishwa na mto huo kukatika kwa muda.

Albetina Kanande amesema mto huo umefurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo kwa muda wa saa mbili na ilipofika saa 12 asubuhi mto ulianza kufurika.

Mkazi mwingine wa eneo hilo, Danny Mwashambwa amesema hali ya kufurika mto huo hujitokeza mara kwa mara.

Kwa upande wake Brigedia Jeneral Mwangela amesema suala hilo atalizungumzia baada ya kuwasiliana na Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads).

"Kwa sasa siwezi kuzungumza chochote kwa sababu sielewi chochote mpaka niwasiliane na meneja wa Tanroads,” amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz