Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mto Ruaha Mkuu haujatiririsha maji miezi mitatu

MTO RUAHA KUKAKUKA Mto Ruaha Mkuu haujatiririsha maji miezi mitatu

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Godwell Ole Meing'ataki amesema kwa takribani miezi mitatu mto Ruaha Mkuu ambao ni tegemeo kwa wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha ambayo ni ya pili Afrika Mashariki, haujatiririsha maji yake hali inayopelekeka wanyama kupata shida na wengine kufa.

Wadau wa uhifadhi na utalii wanasema jitihada za makusudi zinahitajika katika kunusuru uhai wa mto huo ili kukuza sekta ya utalii ambayo huchangia asilimia 17 ya pato la taifa.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego amefanya ziara katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuhamasisha utalii wa ndani na kujionea hali ya sasa ya mto huo ambapo  amekiri serikali itaweka mkazo kuunusuru mto huo.

Mto Ruaha Mkuu kwa sasa hali yake taabani,Wanyama wanateseka ,Hifadhi inayoongoza kuwa na makundi makubwa ya tembo hutegemea mto huu katika kupata maji ya kunywa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live