Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji kikaangoni matumizi ya pombe muda wa kazi

Pombee Ed Mtendaji kikaangoni matumizi ya pombe muda wa kazi

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wameitaka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kumuondoa kazini Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Ukalawa kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ikiwemo ulevi.

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza, Madiwani hao wamesema Mkurugenzi huyo anapaswa kuchukua hatua za kiutumishi dhidi ya mtendaji huyo ambaye anadaiwa kujihusisha na ulevi wa pombe na kusahau majukumu yake.

“Mtendaji huyu sio kijijiji cha kwanza alikuwa kijiji cha Lupembe ameletwa halmashauri amerudishwa Ukalawa na kote ameenda kuharibu, Mwenyekiti kwenye hili tuangalie sheria zinasemaje, hatuwezi kubaki na hawa watu wanatutesa unampata Mtendaji analewa mpaka wananchi wanamshangaa halafu tunaendelea kumbembeleza wa nini?” amesema mmoja wa madiwani

Aidha Ofisa Utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi.Sadala Chota, amethibitisha kuwa Mtendaji huyo ni mlevi na kusema kuwa hatua za awali za kiutumishi zimekwisha chukuliwa.

“Kweli alikuwa anakunywa sana na kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa hiyo malalamiko mengi yalikuja hapa Halmashauri, mtumishi huyu alikiri makosa yake na kuahidi kubadilika na tulimuandikia barua ya onyo kali na itakaposhindikana hatua za juu zaidi zitachukuliwa” amesema Bi.Sadala Chota

Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Valentino Hongoli, amemuagiza Mkurugenzi huyo kuchukua hatua za kinidhamu.

“Mbaya zaidi alikuwa anakunywa wakati wa kazi kwa hiyo tumeazimia kama baraza afunguliwe mashauri ya kinidhamu lakini iwe ni mwisho Mtendaji wa kata au wa kijiji amefanya maasi huko halafu arudi”. Amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live