Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtendaji aliyekimbia kifungo anaswa, atupwa gerezani

29448 Mtenadi+%255Bic TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Jeshi la polisi wilayani Mwanga limemtia mbaroni mtendaji wa kijiji cha Lomwe, Mussa Mteti aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela bila kuwepo mahakamani.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 29,2018  na mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro, Holle Makungu amesema mtuhumiwa aliruka dhamana siku chache kabla kuhukumiwa.

Hata hivyo, Oktoba 31,2018, Hakimu Mkazi wa wilaya ya Mwanga, Mariam Lusewa, alimhukumu mtendaji huyo adhabu hiyo pamoja na faini pasipo kuwapo kortini.

Makungu amesema katika makosa mawili ya ubadhirifu, Hakimu Lusewa alimhukumu mtendaji huyo kulipa faini ya Sh7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.

Katika shitaka la kughushi muhtasari wa kikao cha kamati ya Fedha,Uchumi na Mipango wa kijiji hicho na kujipatia Sh270,000,  Hakimu huyo alimhukumu mtendaji huyo kifungo cha miaka mitano jela.

Adhabu zote zitatumikiwa kwa pamoja,  mtendaji huyo kukamatwa na kupelekwa gereza la Kiruru wilayani Mwanga ili kuanza kutumikia kifungo chake.

Mkuu huyo wa Takukuru aliwaonya washitakiwa wanaopatikana na hatia katika makosa yanayoangukia katika sheria ya rushwa, kutokimbia adhabu zao kwani Serikali ina mkono mrefu na itawatafuta na kuwakamata.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz