Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtambo wa Pesa Bandia wakamatwa Goba

Pesa Bandia Msaoas Mtambo wa Pesa Bandia wakamatwa Goba

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani limewakamata watu wanne wakiwa na pesa bandia za Kitanzania noti 155 za shilingi elfu 10 katika kijiji cha Msata kilichopo Wilaya ya Kipolisi Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Pius Lutumo amesema waliokamatwa ni Mbaraka Fundi (48) na Zena Naringa (42).

Wengine ni Masumbuko Kiyogoma (54) na Elias Wandiba (50) waliokamatwa na pesa nyingine bandia kiasi cha shilingi milioni 12 Aidha, Mtambo wa kutengenezea pesa hizo na zana nyingine vimekamatwa katika makazi ya mmoja wa watuhumiwa hao katika Kata ya Goba Wilaya ya Ubungo, Dar es salaam.

Tazama Picha zaidi hapa chini;





Chanzo: www.tanzaniaweb.live