Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtaka aapa kualiza umasikini Njombe

Mtakataka.jpeg Mtaka aapa kualiza umasikini Njombe

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ametangaza mikakati kuhakikisha mkoa huo unakuwa wa mfano kwa kukuza uchumi na kutokuwa na watu wanaonufaika na Mfuko wa Maendeleao ya Jamii (Tasaf).

Mtaka alisema hayo mjini Njombe kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na anataka kuwa na viongozi wenye ajenda. “Hatuwezi kuwa viongozi tusio na ajenda ya kupambana na umasikini wa watu wetu.

Njombe ni mkoa wenye watu zaidi ya 900 000 lakini una zaidi ya watu masikini 25,000 wanaonufaika na mfuko wa Tasaf,”alisema. Mtaka alisema mkakati wa kuondokana na umasikini pia unalenga kuifanya wilaya ya Makete iwe mzalishaji mkubwa wa ngano nchini.

“Mahitaji ya ngano nchini kwa mwaka ni zaidi ya tani milioni moja kiasi kinachoweza kupatikana kama kutakuwa na mashamba yenye ukubwa wa hekta 600,000. Sisi Makete tumetenga eneo la ukubwa wa hekta 400,000 ili kufikia lengo la kuwa mzalishaji mkuu nchini,” amesema.

Amesema Wilaya ya Makete imepokea tani 80,000 za mbegu kwa ajili ya msimu huu wa kilimo huku wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakiendelea na kazi ya kupima udongo kwa ajili ya kilimo hicho. Aidha, amesema tayari ameanza mpango wa kupunguza idadi ya wanufaika wa Tasaf kwa kuhakikisha kila mnufaika anapatiwa miche 10 ya miparachichi ambayo anatakiwa aitunze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live