Jeshi la polisi Mkoa wa Geita limewaomba na kuwataka wananchi wa Kijiji cha Lulembele kata ya Lulembele wilayani Mbogwe kuacha kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa kwa uchawi bali wapeleke ushahidi kituo Cha polisi ili washughulikiwe kwani sheria ipo.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Safia Jongo wakati Mkutano wa hadhara uliofanyika Katika Kijiji cha Lulembela.
Jongo amesema sheria ya Tanzania inatambua uchawi na sheria ipo hivyo mtu anapomuhisi jirani yake ni mchawi asichukue sheria mkononi bali aripoti kituo cha polisi ili hatua za kumpeleka mahakamani zifuatwe.