Siku chache baada ya Wizara ya Elimu kupiga Marufuku Shule za Bweni kwa Wanafunzi wa Awali hadi Darasa la Nne, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, ameshauri Shule za Bweni kufutwa kabisa kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Kupitia ukurasa wake wa #Twitter, ameandika, "Nashauri Shule za Bweni zingefutwa kwa Shule za Msingi, Secondary na High Schools, ili jukumu la kulea Watoto libaki kwa Wazazi kuepusha Watoto wetu kujifunza mambo ya ovyo yasio ya Maadili ya Kiafrika na Kitanzania, kama Mapenzi ya jinsia moja.”
Siku chache zilizopita Serikali ilipiga marufuku shule za Bweni kwa Watoto wa madarasa ya awali mpaka darasa la nne isipokuwa kwa kibali maalum.