Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msichana anayeumwa kidonda mgongoni atua Muhimbili, atoa neno

53040 BINTI+PIC

Fri, 19 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza kumfanyia uchunguzi Mariam Rajab kubaini chanzo cha kidonda alicho nacho mgongoni.

Taarifa za ugonjwa wa Mariam zilisambaa siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha binti huyo akiomba msaada wa matibabu kufuatia kidonda hicho kilichodumu kwa muda mrefu.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH,  Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 18,2019 amesema hospitali hiyo imechukua jukumu la kumtibia Mariam baada ya kupata maelekezo kutoka wizara ya afya na serikali itabeba gharama zote.

“Tuliona ile video tukafanya juhudi za kumtafuta na hatimaye ametoka Singida tunaye wodini, matibabu yanaendelea na tayari madaktari wamechukua vipimo kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” amesema

Akizungumza akiwa wodini Mariam ameeleza kuwa kidonda hicho amekuwa nacho kwa muda mrefu na amekuwa akikitibia mara kwa mara ila Agosti 2018 kimefuka upya na kumsababishia maumivu makali.

“Nimepitia maumivu kwa muda mrefu nikazungumza na rafiki zangu wakanishauri nitumie njia ya mitandao ya kijamii nashukuru Watanzania wameona na Serikali imeamua kunisaidia,”

Mkuu wa idara ya upasuaji MNH, Ibrahim Mkoma amesema matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa ndiyo yatakayotoa mwongozo ni aina gani ya matibabu ambayo Mariam anatakiwa kupatiwa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz