Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msibabike na wanawake wenye makalio makubwa - DC Songwe

Makalio Makubwa Msibabike na wanawake wenye makalio makubwa - DC Songwe

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Solomon Itunda amewasihi Vijana kuacha kubabaika na kupagawa na Wanawake wenye wenye makalio makubwa (Mizigo) hali inayosababisha kuhonga mpaka mitaji yao ambapo amewakumbusha kuwa baadhi ya mizigo ina gharama zake ikiwemo kufilisi Vijana mitaji na hata kupata magonjwa.

DC Itunda amesema hayo wakati wa kongamano la kujadili namna ya kuzuia ajali Wilayani humo lililowahusisha zaidi ya Vijana 1,000 ambao ni Madereva wa bodaboda, bajaji, guta, noah na taksi lililofanyika katika Mji wa Mkwajuni ambapo amesema wakati mwingine Madereva husababa isha ajali kutokana na kuwaangalia Wanawake hao wakati wao wakiwa wanaendesha.

Amesema wapo baadhi ya Vijana ambao wakipata fedha wanazitumia kununulia pombe na kuhonga mizigo huku wakisahau Familia zao.

“Ndugu zangu tunafanya kazi lakini tunataka tuone matokeo ya kazi mnazozifanya, tunawezaje kufikia hatua hiyo ni lazima tukumbushane Vijana, kuna wakati tumejiingiaza kwenye mazingira mabaya, unakuta unafanya kazi asubuhi mpaka jioni unapata fedha, ukitoka hapo hata nyumbani huendi, kule nyumbani una Mke na Watoto.”

“Vijana wa siku hizi wanachanganywa na mizigo, zamani Vijana walikuwa wanasema tunapenda Mabinti wembamba lakini siku hizi Vijana wengi hasa wa bodaboda wamebadkilika sasa hivi kauli ya mjini ni mizigo, nataka niwaambie mkiona ile mizigo uwe wa kichina au original yote ina gharama zake, wewe umefanya kazi siku nzima ukitoka hapo unakutana na mzigo unategemea kurudi na chochote nyumbani, unahonga mtaji wote kwenye mzigo, unategemea nini kama sio umasikini?”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live