Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msiba wa aliyepumulia mashine ni vuta nikuvute

80734 Msiba+pic Msiba wa aliyepumulia mashine ni vuta nikuvute

Fri, 18 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mpaka mchana wa leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 bado haijajulikana mwili Hamadi Awadh (28) aliyekuwa akiishi kwa zaidi ya mwaka mmoja unusu akipumua kwa msaada wa mashine ni wapi utazikwa.

Marehemu Awadh aliyefariki dunia jana jioni Alhamisi Oktoba 17, 2019 wakati akiendelea kupokea matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila, aliacha wosia kuwa akifariki azikwe na familia ya mke wake Catherine Kulekana ambayo imekuwa ikimuuguza kwa kipindi cha miaka miwili.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Oktoba 18, 2019  Beneth Kulekana ambaye ni baba wa Catherine, nyumbani kwake eneo la Posta-Kipawa jijini Dar es Salaam ambako ndiko msiba ulipo amesema wiki jana marehemu alimuomba amsaidie kuandika wosia ambapo aliomba familia yake isijihusishe na mali wala mazishi yake.

“Ameacha wosia wa maneno na maandishi kwamba asizikwe na familia yake kwa kuwa imeshindwa kumthamini kipindi chote cha ugonjwa wake.”

“Sisi tumelipokea lakini tumetumia busara tumekaa na wenzetu tukashauriana la kufanya na muafaka umefikiwa japokuwa hatujui ujumbe ukifika kwa baba yake Tabata itakuwaje,” amesema.

Baba mkubwa wa marehemu, Mohammed Awadh amesema familia ilipanga msiba ufanyikie Tabata kwa baba yake na mazishi yafanywe kesho Jumamosi saa saba mchana.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Tulipopigiwa simu kwamba mwanenu amefariki, nimekuja hapa kuchukua msiba kuupeleka Tabata alipo baba yake na tumekaa kikao lakini mpaka nifikishe taarifa kwa baba yake ndipo tujue.”

“Kuhusu masuala ya kumtelekeza mimi nilikuwa nakuja kumuona ila tangu Januari mwaka huu nilirudi nyumbani Lindi,” amesema Awadh huku akikataa kujibu sababu ya baba yake Awadh kumtelekeza mwanaye.

Mke wa marehemu Catherine amesema ni vema wakamzika mumewe kwakuwa ameteseka kwa kipindi kirefu, “Wasimsumbue ameteseka sana naomba aoshwe hospitali aswaliwe msikitini akazikwe makaburini.”

Chanzo: mwananchi.co.tz