Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msiba wa Dkt. Ng'wandu mwili waagwa Simiyu (+picha)

WhatsApp Image 2020 12 21 At 12.43.20 660x400.jpeg Msiba wa Dkt. Ng'wandu mwili waagwa Simiyu (+picha)

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Ibada ya kuuaga mwili wa Balozi Dkt. Pius Yasebase Ng’wandu inaendelea muda huu nyumbani kwake Mtaa wa Uzunguni Wilayani Maswa, Simiyu, baada ya kuagwa mwili utasafirishwa hadi Dar Es Salaam kwa ajili ya mazishi.

Dkt.Ng’wandu ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia(2000-2008), amefariki Dunia juzi katika Hospitali ya Somanda, Bariadi Mkoani Simiyu alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Dk Ng’wandu amewahi kuwa Mbunge wa Maswa na pia amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan (1990-1993), na amefariki zikiwa zimepita siku chache tu tangu alipofunga ndoa na Mkewe.

HUZUNI: KILICHOMUUA DKT.NG’WANDU CHATAJWA, NI PRESHA “AMEFARIKI SIKU CHACHE BAADA YA KUFUNGA NDOA”

Chanzo: millardayo.com