Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msiba mama yake Erick Kabendera kufanyika sehemu mbili Bukoba

90775 Kabs Msiba mama yake Erick Kabendera kufanyika sehemu mbili Bukoba

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Msiba wa Varediana Mujwahuzi ambaye ni mama mzazi wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera utafanyika maeneo mawili tofauti Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. Mwili wa Varediana ambaye alifariki Desemba 31, 2019 uliagwa jana Ijumaa jijini Dar es Salaam na leo Jumamosi Januari 4, 2020 utasafirishwa kwenda Bukoba kwa maziko yatakayofanyika Jumatatu ya Januari 6, 2020. Mwili huo utakapowasili leo Jumamosi Bukoba Mjini, utahifadhiwa katika chumba cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera. Akizungumza nyumbani na Mwananchi nyumbani kwao jana Ijumaa Januari 3, 2020, Claudius Kabendera ambaye ni mdogo wake, Erick Kabendera alisema kesho Jumapili mwili wa marehemu utaondolewa hospitalini na kupelekwa eneo la Rwamishenyi alikojenga nyumba yake na kuishi baada ya kustaafu kazi ya ualimu. “Pale Rwamishenyi kutafanyika ibada fupi na mwili wa mama utalala hapo hadi Jumatatu kabla ya kupelekwa kijiji cha Kashenye kata ya Katoma ambako ndiko nyumbani kwao baba,” alisema Claudius Mwananchi ilishuhudia kazi ya kuchimba na kujengea kaburi ikiendelea nyumbani hapo ikiwa ni maandalizi ya maziko yanayotarajiwa kufanyika Jumatatu ya Desemba 6, 2020.

Bukoba. Msiba wa Varediana Mujwahuzi ambaye ni mama mzazi wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera utafanyika maeneo mawili tofauti Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera. Mwili wa Varediana ambaye alifariki Desemba 31, 2019 uliagwa jana Ijumaa jijini Dar es Salaam na leo Jumamosi Januari 4, 2020 utasafirishwa kwenda Bukoba kwa maziko yatakayofanyika Jumatatu ya Januari 6, 2020. Mwili huo utakapowasili leo Jumamosi Bukoba Mjini, utahifadhiwa katika chumba cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera. Akizungumza nyumbani na Mwananchi nyumbani kwao jana Ijumaa Januari 3, 2020, Claudius Kabendera ambaye ni mdogo wake, Erick Kabendera alisema kesho Jumapili mwili wa marehemu utaondolewa hospitalini na kupelekwa eneo la Rwamishenyi alikojenga nyumba yake na kuishi baada ya kustaafu kazi ya ualimu. “Pale Rwamishenyi kutafanyika ibada fupi na mwili wa mama utalala hapo hadi Jumatatu kabla ya kupelekwa kijiji cha Kashenye kata ya Katoma ambako ndiko nyumbani kwao baba,” alisema Claudius Mwananchi ilishuhudia kazi ya kuchimba na kujengea kaburi ikiendelea nyumbani hapo ikiwa ni maandalizi ya maziko yanayotarajiwa kufanyika Jumatatu ya Desemba 6, 2020. Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz