Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Mshikaki wa Bodaboda" waua wanafunzi watano

Kunenge Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, Abubakar Kunenge

Sun, 8 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi watano wa Shule ya Sekondari Kimange wilayani hapa Mkoa wa Pwani wamefariki dunia baada ya pikipiki waliokuwa wamepanda kwa mtindo wa ‘mshikaki’ kugongwa na gari aina ya fuso.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, Abubakar Kunenge amesema kuwa wanafunzi wanne walifariki dunia papo hapo jana usiku baada ya fuso lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es Salaam kuwagonga, huku mmoja akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Jeshi Kihangaiko.

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete amewataja wanafunzi hao waliofariki ni Laya Ubwa Masudi (16), Furaha Athumani (16) na Athumani Mchafu (17) wote wa kidato cha tatu.

Wengine ni Athumani Bushiri (15) na Amina Msomba (15) waliokuwa wanasoma kidato cha kwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigeza amesema:"Ni kweli kuna wanafunzi wamefariki dunia na wote watano walikuwa wamepakizana kwenye pilipiki hiyo moja na walikuwa wamemaliza michezo yao ya kishule kwenye shule jirani ya Kwamakocho wakawa wanarudi makwao."

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa fuso na mwendo kasi kwa kushindwa kumudu gari hilo.

Wanafunzi hao wamezikwa leo Agosti 7, 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live