Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mrisho Mhidini mkazi wa mtaa wa Mwigole kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro amekutwa amefariki Dunia ndani ya chumba chake baada ya kutoonekana tangu Februari 25 mwaka huu.
Aidha, ndugu na majirani wamesema kuwa hadi kufikia sasa hawajafahamu chanzo cha kifo hicho huku wakisema kuwa Marehemu hakuwa na ugomvi na Mtu yeyote na kabla ya kukutwa na Umauti huo Marehemu alikuwa mkoani Lindi katika shughuli zake za ujenzi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro SACP Alex Mkama ameeleza chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika huku uchunguzi wa kina ukiwa unaendelea juu ya tukio hilo.