Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa zaidi ya Tsh. bilioni 23.4 wakwama Singida

RC SINGIDA Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, Amewaomba Wadhamini wa Mradi wa ujenzi wa Ukaguzi wa Pamoja wa Tsh. bilioni 23.4 za kitanzania unaotekelezwa katika wilaya ya Manyoni kufanya Mchakato wa haraka ili mradi huo uanze kutekelezwa.

Dkt Mahenge amesema kuwa Wadhamini hao ndio wenye dhamana ya Kufanya Mazungumzo na Wafadhili husika ambao ni Jumuiya ya Nchi za Umoja wa Ulaya EU Pamoja na Pande zote zinazohusika katika Utekelezaji wa Mradi huo ambao Kimsingi umesimama tangu Mwaka 2018.

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi,CCM Alhaji Juma Kilimba, anasema Mradi Huu iwapo Utakamilika utakuwa na Faida Kubwa kwa Taifa na anaweka wazi Msimamo wa Chama cha Mapindunzi katika Ukamilishaji wa Mradi Huu.

"Mradi huu haukuanzishwa Kwa Bahati Mbaya, Serikali kwa Kushirikiana na Wadau Mbalimbali wa Maendeleo Wanatekeleza Mradi huu Kufuatia Maazimio ya Pamoja ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Africa Mashariki Kupunguza Ucheleweshaji wa Usafirishaji wa Mizigo Kupitia Barabara ya Kati Kuelekea Nchi Jirani za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Demokransia ya Congo" Amesema Mwenyekiti huyo.

Aidha Vituo vya Ukaguzi ambayo vinajengwa katika Mradi huu Ni Manyoni na Nyakanazi na Viko Umbali wa Kilometa 500 Kutoka Kimoja Mpaka Kingine ambapo ujenzi wake Umekwama Kwa Muda kama ambavyo anafafanua Mhandisi Matare Masige Meneja wa Tanroads Mkoa wa Singida.

Mradi huu unasimamiwa na wakala wa Barabara TANROADS ambao pia Wanasimamia Ujenzi wa Barabara ya Itigi hadi Rungwa Mpakani Mwa Singida na Mbeya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live