Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa maji Komuge kupatiwa Sh720 milioni

FEDHA Mradi wa maji Komuge kupatiwa Sh720 milioni

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watumishi wa halmashauri zote nchini kuwa na utaratibu wa kufanya ziara kwenye maeneo yao ili wasikilize changamoto za Wananchi na kuzifanyia kazi.

Ameyasema hayo alipokagua mradi wa maji wa Komuge uliopo halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kutekeleza kampeni yake ya kumtua ndoo Mama kichwani ili kumuwezesha kila Mtanzania kupata huduma ya maji safi na salama karibu na eneo analoishi.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ndani ya wiki hii shilingi Milioni 720 zitatolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji Komuge ili ndani ya miezi mitatu uwe umekamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live