Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi wa bil 520/- neema ya maji Arusha

7e99aa04eb498c202560c71dfd826811 Mradi wa bil 520/- neema ya maji Arusha

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inatekeleza mradi wa maji wenye thamani ya ya Sh bilioni 520 ambao imelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha.

Hatua hiyo ni katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimeelekeza serikali kufikisha maji mjini kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Justine Rujomba alisema jana kuwa mradi huo unatekelezwa kupitia fedha za mkopo wa riba nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Rujomba alisema hayo Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa shughuli za Auwsa na mwelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2022/23.

Alisema hadi kufikia Julai mwaka huu utekelezaji wa mradi mkubwa umefikia asilimia 90.

“Kupitia utekelezaji wa mradi huu, wananchi wa Arusha wameanza kunufaika kwani kiwango cha uzalishaji maji kimeongezeka kwa lita milioni 26 kwa siku na kuchangia kuongezeka saa za huduma kutoka wastani wa saa 15 hadi 19,” alisema Rujomba.

Kwa sasa mahitaji halisi ya maji ni lita 124,789,000 kwa siku ikiwa Jiji la Arusha lita 109,689,250, na miji midogo lita 15,099,750 wakati uzalishaji sasa ni lita milioni 84.5 kwa siku kutoka kwenye vyanzo vya visima virefu, chemchem na mito sawa na asilimia 68 ya mahitaji.

Kabla ya utekelezaji wa mradi huo uzalishaji maji ulikuwa lita milioni 40 wakati uondoaji wa majitaka ilikuwa asilimia 7.6. Rujomba alisema kupitia mradi huo, mamlaka pia imetekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao wa majitaka na ukarabati wa mtandao wa zamani, hatua iliyoifanya maunganisho mapya 4,790 ya wateja wa majitaka.

Alisema pia mamlaka imefanya ukarabati na upanuzi wa mtandao wa majisafi kwa kilometa 600 huku majitaka yakitibiwa kwa asilimia 100 kuendana na viwango vya TBS baada ya ujenzi wa mabwawa 18 ya kutibu majitaka kukamilika eneo la Terati.

Pia wamefunga mtambo wa kupima utendaji kazi wa Dira ambao utumika kupima na kurekebisha dira za wateja zenye changamoto ili kuondoa malalamiko ya wateja kuhusu ufanisi na utendaji kazi wa dira.

“Mamlaka imeweza kuongeza vitendea kazi kama magari, pikipiki pamoja na mitambo mbalimbali na kuongeza ufanisi wa utendaji huku mradi umesaidia upatikanaji wa ajira kwa watu takribani 2,000 kati yao watu 200 ni kutoka nje ya nchi na watu 1,800 kutoka ndani ya nchi,” alisema Rujomba.

Alisema hadi kufikia Juni, mwaka huu wakandarasi wanaotekeleza mradi mkubwa wamenunua vifaa kwenye viwanda vya ndani na maduka ya jumla vyenye thamani ya Sh bilioni 140 huku AUWSA imeajiri watumishi 45 wa kada mbalimbali.

Alisema hadi Juni mwaka huu, mradi umewanufaisha wananchi 1,064 kwa kuwalipa fidia zaidi ya Sh bilioni 5.79 kwa kutwaa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi.

“Pia kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi kimeongezeka kutoka asilimia 66.8 ya wakazi wa Jiji la Arusha mwaka 2020/21 hadi asilimia 75 mwaka 2021/22 huku wateja waliounganishwa wameongezeka kutoka wateja 71,183 Juni 2021 hadi wateja 95,748 Juni 2022,” alifafanua.

Kuhusu mtandao wa majitaka umeongezeka kutoka asilimia 8.03 mwaka 2020/21 hadi asilimia 24 mwaka 2021/22. Aidha, alisema kupitia fedha za ndani Sh milioni 651 wametekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao eneo la Usa River; kujenga chanzo cha Kibola kinachosambaza maji Momela, Arudeko na Bondeni pamoja na kuboresha tangi la DikDik, Magadirisho na Kilimani ambako zaidi ya wateja 4,800 wanaunganishiwa huduma ya maji.

Pia imekamilisha miradi ya maji ya Karatu kwa Tom kwa gharama ya Sh million 623.4, Ayalabe Karatu kwa gharama ya Sh milioni 714.7 na Mradi wa maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Arusha unaofadhiliwa na fedha za UVIKO 19 kwa gharama ya Sh milioni 575.

“AUWSA imefanikiwa kukamilisha utekelezaji wa mradi majisafi wa Namanga, ambao unatokea katika mradi wa majisafi Longido kwa sasa inajenga kilomita 145 za mtandao wa kusambaza maji katika mji wa Namanga,” alieleza.

Aidha, alisema kwa mwaka wa fedha 2022/2023, wamejipanga kutekeleza miradi inayogharimu Sh bilioni 11.8 ya fedha za ndani za ili kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma kwa kujenga mtandao mpya wa majisafi kwa urefu wa kilometa 215.961 katika maeneo mbalimbali.

Kilometa 90 ni maeneo ya Kiserian, Moshono, Murieti, Mkonoo, Laizer, Mtoni, Mlangarini, Safari City, Olmoti, Sokoni I, kilometa 36.1 kutoka Olmoti na tangi la Murriet kwenda Bondeni City; kilometa 35.5 Mji wa Monduli; kilometa 13.8 mji wa Usa River; kilometa 30.561 Mji wa Ngaramtoni na kilometa 10 mji wa Longido.

Pia kuunganisha wateja wapya 13,993 kati ya hao wateja 10,893 katika Jiji la Arusha, na wateja 3,100 miji midogo, kuongeza mtandao wa majitaka kwa kilometa 10 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha na kuunganisha wateja 4,200 katika huduma ya uondoaji wa majitaka.

Pia kujenga chemba 1,237 za kuhifadhia dira za wateja ili kudhibiti uharibifu na wizi wa dira za maji na maji na kuboresha mtandao chakavu wa majisafi katika maeneo mbalimbali kwa kilomita 64 jiji la Arusha, na miji midogo kilometa 40.7.

Nyingine ni kuendelea kutunza na kujenga vyanzo vya maji vinavyotumika jijini Arusha pamoja na miji midogo; kuendelea na maboresho ya matangi ya kuhifadhia maji na kujenga mapya Monduli yenye ujazo wa lita 500,000 Mlimani Mashariki na lita 300,000 Lengine Juu; kujenga tangi la ujazo wa lita 1000,000

Chanzo: www.tanzaniaweb.live