Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi bonde Msimbazi kuanza Aprili 2023

Msimbazi Pic 2023 Mradi bonde Msimbazi kuanza Aprili 2023

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari njema kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam baada ya Serikali ya Tanzania kuthibitisha rasmi kuanza utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Msimbazi Aprili 2023.

Hatua hiyo imethibitishwa jana Jumatatu Novemba 21, 2022 wakati wa utiaji saini kati ya Serikali na Benki ya Dunia inayotoa mkopo wa riba nafuu dola 535milioni, sawa na Sh1.2 trilioni.

Katika makubaliano hayo, Serikali imepokea mkopo kwa ajili ya miradi miwili: mkopo wa dola 335 milioni (Sh777.17 bilioni) kwa ajili ya kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) na dola 260milioni (463.98 bilioni) kwa ajili ya mradi wa bonde hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Rogatus Mativila amesema kazi itakayoanza kwa sasa ni kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata mkandarasi atakayejenga bonde hilo.

“Kwa kawaida zabuni hufanyika ndani ya miezi mitatu kwa hiyo tunatarajia ujenzi rasmi uanze Aprili mwakani na mradi tunatarajia ufanyike ndani ya miaka miwili hadi mitatu,”amesema Mativila.

Kwa mujibu wa Tanroads, urefu wa daraja utakuwa mita 390 na kimo chake mita saba kutoka usawa wa bonde hilo.

Awali, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema; “kati ya hizo dola 260milioni, kuna dola 30milioni msaada kutoka Uholanzi na mkopo wa dola 30 milioni kutoka Hispania, tunawashukuru sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live