Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mradi BRT watajwa kuchochea ukuaji uchumi

10332 Brt+pic TZW

Sat, 30 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kuinua uchumi wake iwapo itaendelea kuimarisha usafirishaji katika miji kama ilivyo mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) unaochochea maendeleo na kuimarisha uzalishaji.

Mbombezi wa sera za usafirishaji na matumizi ya ardhi, Profesa Genevieve Giuliano wa Chuo Kikuu cha Southern California nchini Marekani alisema hayo jana katika mkutano wa kimataifa wa siku tatu unaofanyika jijini hapa kujadili usafirishaji endelevu katika majiji ulimwenguni.

Giuliono alisema Tanzania ipo kwenye nafasi nzuri kutokana na wingi wa rasilimali ilizonazo.

“Pia utulivu wake wa kisiasa unaipa nafasi kubwa kufanya shughuli za maendeleo kama mradi huu wa usafirishaji ambao unaokoa muda wa safari kwa Watanzania kwa kiasi kikubwa.

“Huwa ni vigumu kwa nchi zenye kipato kidogo kuboresha mifumo yao ya usafirishaji kwa umma kutoka na kukosa rasilimali fedha,” alisema Giuliano ambaye amefanya tafiti zaidi ya 100 na kuandika vitabu 40 kuhusu usafirishaji na matumizi ya ardhi. Alisema kuanzishwa kwa sera, sheria na miongozo mbalimbali, BRT inaweza kushamiri katika miji na kukuza sekta ya usafirishaji ujumla.

Chanzo: mwananchi.co.tz