Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango ataka umeme wa gridi Kigoma mwakani

602fcdd22a70bc2c71919cfd04ed3749 Mpango ataka umeme wa gridi Kigoma mwakani

Fri, 16 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lihakikishe umeme wa gridi unafika mkoani Kigoma mwakani.

Dk Mpango alitoa agizo hili jana wakati akizindua ujenzi wa kituo cha kupokea umeme wa gridi kutoka mkoani Tabora.

Alisema ukosefu wa umeme wa uhakika umesabanisha Mkoa Kigoma ushindwe kutekeleza mpango wa maendeleo ya viwanda.

Dk Mpango alisema sasa inatosha kuona mkoa huo ukiteseka kwa matatizo ya umeme.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, alisema mradi huo utakamilika mwaka 2023 na kwamba megawati 32 zitazalishwa.

Byabato alisema mradi huo unatekelezwa kwa kutumia wahandisi wa ndani kutoka Tanesco na kwamba umeme utasafirishwa kwa kilometa 395 kutoka Urambo mkoani Tabora.

Alikiri kwamba kwa sasa Mkoa wa Kigoma unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa kuwa jenereta za kuzalisha umeme zimechakaa na hivyo utekelezaji wa mradi huo utasaidia kuondoa tatizo hilo.

Dk Mpango alisema ni lazima Wizara ya Nishati isimamie mradi huo ukamilike haraka ili wananchi wa mkoa huo wapate umeme wa gridi ya taifa.

Alisema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoeleza kuwa serikali utapeleka umeme wa gridi mikoa yote nchini sambamba na kuongeza uzalishaji wa umeme utakaopelekwa vijiji vyote nchini.

Dk Mpango aliitaka Tanesco ihakikishe watu wote ambao maeneo yao yanapitiwa na njia ya kusafirisha umeme kwenda mjini Kigoma wanalipwa fidia.

Alitoa tahadhari kwa wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 kwa kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa 10 yenye wagonjwa wengi.

Dk Mpango alisafiri kwa gari kwenda kufanya ziara mkoani Kigoma akitoka Dodoma na alisema alifanya hivyo ili aione nchi vizuri.

Chanzo: www.habarileo.co.tz