Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpanda: Mtoto wa miaka 10 auawa akiwa machungani

Mtoto Auawaaaa Mpanda: Mtoto wa miaka 10 auawa akiwa machungani

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa Miaka 10 kutoka Kijiji cha Kakese Kata ya Kakese Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ameuwawa na Watu ambao hawajatajwa majina wakati akiwa kuchunga ng'ombe.

Akiwa kaitka mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kakese kata ya Kakese, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf amesema tukio hilo limetokea Oktoba 24, 2022 wakati mtoto huyo akiwa machungani na ndipo alipokutana na watu hao kwa lengo la kuiba ng'ombe wanne waliokuwa wakichungwa na Mtoto huyo.

"Pengine aliwatambua na wenyewe wakamtambua kwa hiyo wakaona ili kufanya namna gani iishe ni kufanya ukatili kwa kiumbe kile."

Hata hivyo, DC Jamila amesema Ng'ombe hao wamepatikana na wahusika wote wamekamatwa.



DC Jamila ametoa pole kwa familia iliyokumbwa na kadhia hiyo huku akiwaahidi Wananchi kuwa Serikali itaimarisha ulinzi na wote wanaovunja Sheria watachukuliwa hatua.

Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji hicho wameililia Serikali kuona namna wanaweza kujengewa kituo cha Polisi kwani usalama Kijijini hapo umekuwa mdogo kutokana na wizi kushamiri vikiwemo vitisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live