Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto waweka hatarini ajira za wahandisi Tanesco

Dk Kalemani Dk Kalemani Waziri wa Nishati na Madini

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewasimamisha kazi wahandisi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupisha uchunguzi baada ya Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme Msamvu kuungua moto na kusababisha hasara ya takribani shilingi Bilioni 2.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo, Mkoani Morogoro, Agosti 03, 2021 alipofanya ziara ya kukagua kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msamvu kilichoungua moto Jana baada ya kutokea hitilafu na kusababisha wananchi kukosa Umeme.

Wahandisi hao wa TANESCO, wamesimamishwa kwa kushindwa kubaini hitilafu iliyotokea katika mifumo ya kuendeshea mitambo kituoni hapo, na kusababisha harasa kubwa kwa taifa baada ya kituo hicho kuungua moto.

Aidha amemuagiza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali kuunda kamati ya kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha Moto huo na hasara iliyopatika ndani ya siku tano kuanzia leo (Agosti 3, 2021).

Hata hivyo aliitaka TANESCO kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha umeme unarejea katika maeneo yote ndani ya saa 24 kuanzia leo,vilevile waongeze wataalam kutoka vituo vingine ili kuongeza nguvu kazi na kukamilisha kazi hiyo haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live