Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Moto wateketeza nyumba, watu 35 wakosa mahali pa kuishi

Moto Morogoro Moto wateketeza nyumba, watu 35 wakosa mahali pa kuishi

Mon, 12 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 35 kutoka kaya 13 waliokua wakiishi kwenye nyumba moja ya kupanga mtaa wa Makaburi C manispaa ya Morogoro wamekosa mahali pakuishi baada ya Nyumba waliyokua wakiishi kuteketea kwa Moto unaodaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro ACP. Ralph Meela hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu uharibifu uliojitokeza ni Nyumba iliyoteketea pamoja na vitu vyote vilivyokua ndani ya Nyumba.

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo ndio wameongoza zoezi la uokozi, ambapo wamesema mpaka sasa bado thamani halisi ya Mali zilizoteketea haijatambukulika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live